Isimujamii
  • Authors: P. I. Iribemwangi & Ayub Mukhwana
  • ISBN: 9966-01-152-8
  • Units in Stock: 1000
  • Published by: Focus Publishers
epub

 

View Flipbook

 

flipbook

Price:   Ksh. 400.00

Add to Cart:          

 

Book Details:

 

Isimujamii ni kitabu kinachoangazia maswala ya mahusiano yaliyopo baina ya lugha na jamii na vilevile jinsi jamii inavyotumia lugha. Mada za kitabu hiki zinahusu maelezo ya taaluma ya isimujamii, umuhimu wake na jinsi ambavyo masiala mbalimbali yanavyopelekea matumizi ya lugha kujipambanua. Kitabu chenyewe kinafafanua maswala mengi yanayohusu lugha na jamii. Juu ya hayo, kitabu hiki pia kinaangazia dhana muhimu zitumiwazo katika taaluma ya isimujamii kama vile lugha, lahaja, lafudhi, sajili na msimbo. Jambo lingine muhimu ambalo limefafanuliwa ni ujuzi wa lugha katika jamii ambapo mambo kama umojalugha, uwililugha, wingilugha, daiglosia nk yanajitokeza. Katika Isimujamii pia kuna maelezo juu ya majukumu ya lugha katika jamii, upangaji lugha na sera ya lugha. Haya ni mambo ambayo kwa muda mrefu hayakutiliwa umuhimu yanayostahiki hususani katika asasi zetu za elimu. Hili ni pengo kubwa hasa ikichukuliwa kuwa lugha ni mali ya jamii na kwamba kuna uwezekano wa kutokuwepo lugha kama jamii haipo. Kitabu hiki kinakusudiwa kusaidia kujaza pengo hili. Kwa sababu hiyo, Isimujamii ni nguzo muhimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu (katika viwango vya shahada ya kwanza na uzamili), wa vyuo vya ualimu na pia wale wa shule za upili. Kitabu hiki pia kitawafaa walimu wa Kiswahili pamoja na wote wanaokienzi Kiswahili.The Authors
P. I. Iribemwangi ni mwanaisimu, mwandishi, msomi na mwalimu mwenye tajriba pevu katika ufundishaji wa Kiswahili. Dkt. Iribemwangi alisomea katika Chuo Kikuu cha Nairobi alikohitimu na Shahada ya Elimu na Sanaa (B.Ed, Arts), Shahada ya Uzamili katika Kiswahili (M.A) na hatimaye Shahada ya Uzamilifu (PhD) katika Isimu ya Kiswahili. Kwa sasa yeye ni mhadhiri wa isimu ya Kiswahili katika Idara ya Isimu na Lugha ya Chuo kicho hicho. Pamoja na kazi yake ya uhadhiri, Dkt. Iribemwangi ni mtaalam wa tafsiri na pia ni mchambuzi wa vitabu na maswala ya siasa katika vyombo mbalimbali vya habari. Vilevile, ameandika vitabu kadhaa kikiwepo The Structure of Kiswahili: Sounds, Sound Changes and Words (VDM Verlag, Ujerumani). Kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu kama mhadhiri, Iribemwangi alifundisha Kiswahili katika shule za upili zifuatazo: Salama, Njoro Boys’, Mugumo na Mutige. Ayub Mukhwana ni mwalimu wa Kiswahili mwenye uzoevu mkubwa. Amefundisha Kiswahili katika shule za upili za Lugari na Malava mkoani Magharibi pamoja na Loreto Convent Msongari na City High School mkoani Nairobi. Kwa sasa, Dkt. Mukhwana ni Mhadhiri katika Idara ya Isimu na Lugha ya Chuo Kikuu cha Nairobi. Amewahi pia kufunza katika Chuo Kikuu cha Maseno na katika Chuo Kikuu cha walimu cha Tianjin Normal University nchini Uchina. Ayub Mukhwana ana shahada za B.A na M.A katika Kiswahili na pia shahada ya PhD katika Isimujamii kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.