Fasihi Andishi na Simulizi
  • Authors: P. I. Iribemwangi, Kariuki Chege & Betty Kiruja
  • ISBN: 9966-01-152-8
  • Units in Stock: 1000
  • Published by: Focus Publishers
epub

 

View Flipbook

 

flipbook

Price:   Ksh. 0.00

Add to Cart:          

 

Book Details:

 

Fasihi Andishi na Simulizi ni kitabu kinachotalii fasihi hasa kwa kurejelea lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki kinafafanua maana, jukumu na umuhimu wa fasihi. Hiki ni kitabu kinachouchanganua uwanja mzima wa fasihi ikiwa ni pamoja na kuchunguza fasihi andishi na pia fasihi simulizi. Juu ya hayo, hiki ni kitabu kinachochunguza mbinu mbalimbali za fasihi na mambo kama vile uhusika, msuko na ploti. Katika fasihi simulizi, waandishi wamechanganua tanzu tofautitofauti; kwa mfano, wameeleza aina mbalimbali za hadithi, ushairi simulizi, nyimbo na semi za aina tofauti. Vilevile, waandishi wamechunguza kwa kina tanzu za fasihi andishi kama vile riwaya, tamthilia, hadithi fupi na ushairi. Kwa kila mojawapo wa tanzu hizi, waandishi wametoa ufafanuzi uliokolea, kueleza mbinu za uchambuzi na kutoa mifano chungu nzima. Kitabu hiki kinatoa maelezo yenye kina kwa njia sahili inayoeleweka kwa urahisi. Mpangilio uliotumiwa unakifanya kitabu hiki kiwe na upekee wake. Kutokana na hayo, inadhihirika kwamba Fasihi Andishi na Simulizi ni kitabu muhimu cha rejea kinachoweza kutumika katika vyuo vikuu, vyuo na pia katika shule za upili. Ni kitabu muhimu kwa walimu wa Kiswahili na wapenzi wote wa fasihi na lugha ya Kiswahili.The Authors
P. I. Iribemwangi ni mwanaisimu, mwandishi, msomi na mwalimu mwenye tajiriba pevu katika ufundishaji wa Kiswahili. Ana shahada za B.Ed, M.A na PhD kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. Kwa sasa yeye ni mhadhiri mwandamizi wa Kiswahili katika Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Nairobi. Pamoja na kazi yake ya uhadhiri, Dkt. Iribemwangi ni mtaalam wa tafsiri na pia ni mchambuzi wa vitabu na maswala ya siasa katika vyombo mbalimbali vya habari. Ameandika vitabu vingi vikiwepo Isimujamii (Focus Publishers Ltd), Alidhani Kapata na Hadithi Nyingine (EAEP), Kunani Marekani na Hadithi Nyingine (Target), Othello (Oxford, Tafsiri) na Human Rights, African Values and Traditions: An Inter-disciplinary Approach (Focus Publishers Ltd) kati ya vingine. Kariuki Chege ana shahada za ualimu za B.Ed kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na M.Ed kutoka Chuo Kikuu cha Moi. Yeye ni mwalimu wa lugha na fasihi ya Kiswahili mwenye tajriba na uzoevu mpana na wa kina. Ni mtahini mkomavu wa kitaifa aliyebobea katika utahini wa somo hili. Mbali na kufunza Kiswahili katika shule nyingi, Bw. Chege pia amekuwa Mwalimu Mkuu wa shule kadhaa za upili na kwa sasa yeye ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Upili ya Naaro, Mathioya katika Kaunti ya Kandara. Betty Kiruja ana shahada za B.Ed na M.A katika Kiswahili kutoka vyuo vikuu vya Moi na Nairobi mtawaliwa. Amekuwa mwalimu wa lugha na fasihi ya Kiswahili kwa miaka mingi katika shule mbalimbali humu nchini. Pia, amefundisha Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Nairobi katika Kitivo cha Masomo ya Mbali. Bi. Kiruja ni mwandishi anayeinukia na amewahi kuchapisha hadithi fupi kadhaa.