Fahali Mtoboa Siri
  • Authors: Bitugi Matundura
  • ISBN: 9966-01-112-9
  • Units in Stock: 1000
  • Published by: Focus Publishers
epub

 

View Flipbook

 

flipbook

Price:   Ksh. 185.00

Add to Cart:          

 

Book Details:

 

SIFA za jiji la Madongokuinama zilianza kupotea moja baada ya nyingine. Mito yake iliyokuwa na maji safi na baridi kama barafu ilianza kukauka. Misitu yake iliyokuwa na miti mbalimbali ilianza kushambuliwa ghafla na wanajiji walafi waliojinyakulia ardhi. Hatimaye kiangazi kilichoandamana na njaa kubwa kikatokea. Mzee Jumbe, tabibu maalumu wa kienyeji aliathiriwa sana na matokeo hayo ya uharibifu wa kimazingira. Ukame uliotokana na ukataji ovyo wa miti ulisababisha kutoweka kwa dawa za mitishamba ambazo alizitegemea sana katika taaluma yake. Dawa kadha za kienyeji au mitishamba zilizokuwa zinapatikana kwa wingi na urahisi katika misitu ya jiji la Madongokuinama zilipotea ghafla kama umande kwenye jua la asubuhi. Zikawa adimu kupatikana lilivyo kaburi la Baniani.The Authors
Bitugi Matundura