Kiswahili Readers


Isimujamii ni kitabu kinachoangazia maswala ya mahusiano yaliyopo baina ya lugha na jamii na vilevile jinsi jamii inavyotumia lugha. Mada za kitabu hiki zinahusu maelezo ya taaluma ya isimujamii, umuhimu wake na jinsi ambavyo masiala mbalimbali yanavyopelekea matumizi ya lugha kujipambanua.


Product Image Item Name-

Jogoo na Kanga

Description

Author(s): Gora Haji Gora

ISBN: 9966-01-086-6

Jogoo amemuacha rafiki yake akaenda kwa binadamu kutafuta moto. Kanga amesikitika, kwani baridi ni kali. Je, Jogoo ataleta moto?....

Ksh.100.00

Add:

 

Elimika: Epuka Janga la Ukimwi

Description

Author(s): Joe Babendreier

ISBN: 9966-01-081-3

Kitabu hiki kiliandikwa kwa manufaa ya vijana, ambao wangetaka kufahamu mengi zaidi, juu ya jinsia zao za kike au za kiume, na pia kuijua sababu hasa ambayo Mungu aliwaumba, wakiwa wa jinsia hizo. Kwa vile kufikia sasa watu wote wanajua hatari ya Ukimwi, na jinsi ulivyoenea, kitabu hiki kinaanza kwa kurejelea mambo ya msingi ya matibabu ya Ukimwi. Hata hivyo mtazamo wa kitabu hiki unalenga mbali zaidi, kuliko kulishughulikia janga hili kama lilivyo sasa hivi tu.....

Ksh.175.00

Add:

 

Binti Mfalme na Chura

Description

Author(s): Collins Mdachi

ISBN: 9966-01-083-1

Hadithi inatufundisha kuwa wema kwa watu wanaotutendea mema. Pia ni vizuri kutimiza ahadi tunazotoa kwa wengine.....

Ksh.100.00

Add:

 

Alitoroka Kwao

Description

Author(s): Angelina Mdari

ISBN: 9966-882-59-6

Lo! Mara Eva alipoipokea ile risiti yake akaanza kutetemeka kwa woga. Akajiwa na fikira zilizomzomea, ‘Mtoto umepotea wewe! Ati unaenda Nairobi? Unamjua nani huko? Nani anayekujua huko?’ Mawazo hayo yakamjaa ubongoni. Eva akaendelea kutetemeka kwa hofu. Na kweli, huko alikokokuwa anakwenda alimjua nani? Lakini hapana! Akajipa moyo tena. Hangerudi nyuma! ....

Ksh.150.00

Add:

 

Yasinya

Description

Author(s): Leornard Sanja

ISBN: 9966-01-158-7

Nyumba nzuri, nyumba ya fahari, lakini nyumba ambayo ilimliza badala ya kumpa fahari, furaha na raha kuwa na nyumba. Kisura alikuwa amelala ndoto ya M A na hadithi zilipomhusu zilipomjia. Je, atavumbua na kufumbua kitendawili cha nyumba? Atarejesha hahari na ari ya nyumba ili raha irejee? Ama naye atasinyika? Yasinya ni riwaya inayochunguza masuala yanayozitatiza na kuzidunisha nchi nyingi barani na kuzifanya zikose mshikamano, ustawi na maendeleo. Baadhi ya mambo anayoyaangazia mwandishi ni ukiritimba, umaskini na ukabila.....

Ksh.340.00

Add:

 

Yalianza Kimchezomchezo

Description

Author(s): Angelina Mdari

ISBN: 9966-882-63-4

Yalianza Kimchezomchezo Mambo mengine huanza kama mchezo halafu yakaishia si mchezo bali ni hatari. Rita alianza kimchezomchezo kuangalia picha mbovu. Soma uone yaliyompata yeye na rafiki yake Suzzy.....

Ksh.110.00

Add:

 

Isimujamii

Description

Author(s): P. I. Iribemwangi & Ayub Mukhwana

ISBN: 9966-01-152-8

Isimujamii ni kitabu kinachoangazia maswala ya mahusiano yaliyopo baina ya lugha na jamii na vilevile jinsi jamii inavyotumia lugha. Mada za kitabu hiki zinahusu maelezo ya taaluma ya isimujamii, umuhimu wake na jinsi ambavyo masiala mbalimbali yanavyopelekea matumizi ya lugha kujipambanua ....

Ksh.400.00

Add:

 

Kunganyira

Description

Author(s): Haji Gora Haji

ISBN: 9966-01-085-8

Kunganyira ni maskini anayetegemea ukarimu wa jirani na marafiki. Siku aliyopata kitoweo Kunganyira alichukia ukarimu, akaona kwamba ukarimu ni uonevu! Ni nini kilimtokea baada ya hapo?....

Ksh.150.00

Add: