Focus Logo

Your Shopping Cart




Your Cart is currently empty.

   

Info: Your browser does not accept cookies. To put products into your cart and purchase them you need to enable cookies.
PDFPrintE-mail


Kunga Za Kiswahili Kidato 2
View Full-Size Image


Kunga Za Kiswahili Kidato 2

( Focus Publishers )
ksh 400.00


Waandishi: Timothy Arege, Assumpta Matei

ISBN: 9966-01-007-6

Kunga za Kiswahili ni mfululizo wa vitabu vya Kiswahili ambavyo vinashughulikia masuala mbalimbali ya lugha na fasihi kulingana na mahitaji ya mtaala mpya wa Kiswahili nchini Kenya. Vipengele mbalimbali vimeshughulikiwa kwa namna ambayo inamwezesha mtumiaji wa vitabu hivi kupata maarifa yaliyomo bila kujidhiki. Pamoja na kufunza stadi mbalimbali za lugha, kitabu kinashughulikia kwa kina masuala ibuka yanayoiathiri jamii. Haya ni pamoja na masuala ya kijinsia, janga la ukimwi, maadili, ajira na haki za watoto.

Mazoezi yaliyomo yanamwezesha mwanafunzi kujitathmini mwenyewe katika viwango mbalimbali kama vile ujuzi, ufahamu, uchanganuzi, usanisi, utathmini na matumizi. Pamoja na haya, mazoezi yenyewe yanasaidia kukuza stadi za kuzungumza, kusoma na kufahamu ambazo ni miongoni mwa malengo ya silabasi mpya.

Waandishi wa kitabu hiki ni wataalamu waliobobea katika lugha na fasihi ya Kiswahili.

Timothy Arege ana tajribaya kufundisha somo la Kiswahili. Miongoni mwa shule alizofundisha ni shule ya wasichana ya Gekano na shule ya wasichana ya Limuru. Pia amefundisha katika Chuo Kikuu cha Nairobi na Chuo Kikuu cha Maseno. Kwa sasa Timothy M. Arege ni mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu Katoliki cha Afrika Mashariki (Catholic University of Eastern Africa). Timothy Arege ni Mwandishi wa hadithi fupi na mashairi. Pia ameandika Mwongozo wa Mayai Waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine na Mwongozo wa KifoKisimani.

Bi Assumpta Matei ni mwalimu mwenye tajriba ya miaka mingi. Amekuwa akifundisha lugha na fasihi ya Kiswahili katika shule ya upili ya Kenya High. Ameshiriki katika majopo mbalimbali ya ukuzaji na utekelezaji wa mtaala, mojawapo ikiwa jopo la kitaifa la Utathmini wa Vitabu Vinayotumiwa Shuleni.





Customer Reviews:

There are yet no reviews for this product.
Please log in to write a review.