Focus Logo

Your Shopping Cart




Your Cart is currently empty.

   

Info: Your browser does not accept cookies. To put products into your cart and purchase them you need to enable cookies.
PDFPrintE-mail


Kurunzi ya Kiswahili (KCSE Kitabu cha Marudio)
View Full-Size Image


Kurunzi ya Kiswahili (KCSE Kitabu cha Marudio)

( Focus Publishers )
ksh 560.00


Waandishi: Sanja Leonard Leo, Kusino M. Tonny

ISBN: 9966-01-048-3

Kitabu cha Marudio kimeandikwa kwa madhumuni ya kuondolea mbali hali ya taharuki miongoni mwa wanafunzi na walimu kuhusu matarajio ya silabasi mpya. Yaliyopewa kipaumbele ni mahitaji ya mwanafunzi katika kuukabili mtihani wa sampuli yoyote ile.

Waandishi wamepembua kwa mapana na marefu vipengele vyote vya silabasi mpya kwa njia sahili, fupi na rahisi kufuatia. Aidha, wametoa mifano ya karatasi za maswali zinazotoa taswira kamili ya mtihani wa K.C.S.E. Yote hayo yamefanywa kwa mtindo mufti ambao bila tashwishi utasadifu wanafunzi wa viwango vyote: wepesi darasani na wanaojifunza asteaste.

Baadhi ya vipengele muhimu vilivyoshughulikiwa kwa kina ni:

  • Uandishi wa insha
  • Ufahamu na ufupisho
  • Isimu-jamii
  • Matumizi ya lugha (sarufi)
  • Uchanganuzi wa sentensi
  • Fasihi simulizi na andishi
  • Uchambuzi wa vitabu teule (riwaya, tamthilia na hadithi fupi)pamoja na mashairi
  • Namna ya kujibu maswali ya sampuli zote.
  • Majaribio ya mitihani yenye sura tarajiwa ya K.C.S.E. silabasi mpya.

Bwana Sanja Leonard Leo ana shahada ya digrii kutoka Chuo Kikuu cha Moi. Amefunza kwingi zikiwemo shule za Kitengela Girls na ile ya Kitaifa ya Limuru Girls. Aidha ameshiriki katika kipindi cha KBC 'Lugha Yetu' kwa miaka mingi.

Bwana Kusino M. Tonny ana digrii ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi. Amefunza kwingi zikiwemo shule maarufu za Bulimbo Girls na Makunda Muslim. Ameshiriki katika warsha tumbitumbi za kutathmini miswada ya vitabu mbalimbali vya silabasi mpya. Warsha hizi zimemweka katika nafasi aula ya kuelewa jinsi mtihani wa silabasi mpya utakavyotahiniwa.





Customer Reviews:

There are yet no reviews for this product.
Please log in to write a review.