Ramatoulaye, mwanamke Msenegali ameolewa na Modu, mtu mzito serikalini. Baada ya miaka mingi ya ndoa Modu anaoa mke mwingine, msichana mdogo mwenye umri sawa na binti yake. Ramatoulaye anasahauliwa; pesa na mapenzi vinahamia kwa mke mdogo. Modu anakufa katika ajali ya gari. Nani atakayerithi mali ya marehemu? Halafu kuna umati uliokuja kwenye kilio ambao lazima ulishwe na upewe pesa kwa…
Kichocheo cha Fasihi; Simulizi na Andishi ni kitabu kilichoandikwa kwa mtindo mwepesi na rahisi kusomeka. Kitabu hiki kinachunguza vipengele vya kimsingi vya fasihi simulizi na fasihi andishi kwa undani unaopatikana kwa nadra sana katika vitabu vilivyochapishwa.
Kielezi cha Tungo ni kitabu kinachojadili kwa mapana namna ya kuandika tungo mbalimbali. Hiki ni kitabu cha kipekee ambacho kimeangazia aina mbalimbali za tungo kwa kina. Mwandishi huyu anatoa mifano maridhawa katika kila utungo anaoushughulikia. Kina sehemu zinazoshughulikia maana na aina za insha, tungo amilifu, tungo za kifasihi, ufahamu na ufupisho. Aidha amelijadili kwa mapana swala la uakifishi. Kitabu hiki…