Barua Ndefu Kama Hii

KSh350.00

Ramatoulaye, mwanamke Msenegali ameolewa na Modu, mtu mzito serikalini. Baada ya miaka mingi ya ndoa Modu anaoa mke mwingine, msichana mdogo mwenye umri sawa na binti yake. Ramatoulaye anasahauliwa; pesa na mapenzi vinahamia kwa mke mdogo. Modu anakufa katika ajali ya gari. Nani atakayerithi mali ya marehemu? Halafu kuna umati uliokuja kwenye kilio ambao lazima ulishwe na upewe pesa kwa heshima ya marehemu.

100 in stock

Category:

Description

Katika Barua Ndefu Kama Hii Ramatoulaye anayatafakari maisha yake na jamii ya Kiislamu ya Senegal kufichua shida na mashaka yanayowasibu wanawake wote wa Kiafrika bila kujali dini wala nchi wanakotoka.

Mariama Bâ, mwandishi wa riwaya hii, alikuwa wa kwanza kupewa tuzo ya NOMA mwaka wa 1980. Riwaya hii imetafsiriwa katika lugha kumi na nane na umaarufu wake unazidi kukua.

Additional information

Author

Miriama Ba