Elimika: Epuka Janga La Ukimwi

KSh175.00

Elimika: Epuka Janga La Ukimwi
Mwandishi: Joe babdenreier
Tafsiri:Angelina Mdari

SKU: ISBN 9966-01-081-3 Category: Tag:

Description

Kitabu hiki kiliandikwa kwa manufaa ya vijana, ambao wangetaka kufahamu mengi zaidi, juu ya jinsia zao za kike au za kiume, na pia kuijua sababu hasa ambayo Mungu aliwaumba, wakiwa wa jinsia hizo. Kwa vile kufikia sasa watu wote wanajua hatari ya Ukimwi, na jinsi ulivyoenea, kitabu hiki kinaanza kwa kurejelea mambo ya msingi ya matibabu ya Ukimwi. Hata hivyo mtazamo wa kitabu hiki unalenga mbali zaidi, kuliko kulishughulikia janga hili kama lilivyo sasa hivi tu.
Hoja ya muhimu sio tu namna ya kupambana na hili tatizo baya. Muhimu zaidi, ni jinsi ya kulielewa hili fumbo linaloitwa jinsia. UKIMWI ni maafa yanayotisha, kwa sababu, ghafia bin vuu! umekuwa ndio ugonjwa mmoja unaowaua watu wengi zaidi ulimwenguni, hasa kwenye sehemu fulani fulani zenye watu wengi sana. Uume na uke wa binadamu ni mojawapo ya sura nzuri sana za maumbile na uwepo wetu, na pia ni mojawapo ya fumbo kubwa sana la kuumbwa kwa mwanadamu. Ingawa hatutaweza kulielewa fumbo hili la jinsia zetu kikamilifu, ni kweli kuwa kadiri tunavyojaribu kulielewa zaidi, ndivyo tutakavyoweza kupambana na hili janga la ukimwi, pamoja na majanga mengine mabaya kama hili, ambayo yanatishia maisha yetu.
Sehemu ya pili ya hiki kitabu inaongea juu ya ndoa na jinsi ya kujitayarisha kwa ndoa. Mambo hayo yameshughulikiwa kwa mtazamo wako wewe kijana, ukiwa ni mtu ambaye bado unayo mambo mengi sana, ya kuyazingatia katika hali na maisha yako unayoishi sasa.
Maneno yasiyo ya kawaida sana yameelezwa mwishoni mwa kitabu. Maelezo hayo yametolewa kulingana na vile yalivyotumika humu ndani. Tunakutakia usomaii mwema ili uupate ujumbe, uelimike ulivyo, uusambaze na uliepuke janga lililovamia ulimwengu.