Fahali Mtoboa Siri

KSh185.00

Fahali Mtoboa Siri
Mwandishi: Bitugi Matundura

Description

Fahali Mtoboa Siri ni hadithi ya kuvutia kumhusu
Kombo, mvulana mdogo anayejipata kapotelea
msituni. Anaokolewa na Mzee Jumbe, ambaye
anampeleka kwake na kumtunza hadi anakua na kufikia
umri wa kuwachunga mifugo wa Mzee huyo. Mzee
Jumbe anapogundua kuwa Kombo anakumbuka kwao
iliko, anahofia kuwa atapata hasara kubwa endapo
Kombo ataondoka kwenda kwao hasa baada ya kumlea
kwa miaka mingi. Anafanya mikutano ya kisirisiri
kupanga njama na wake zake ili wamuue Kombo.

Bitugi Matundura ni mwandishi wa hadithi fupi na
vitabu vya watoto. Kazi zake ni kama vile Mkasa wa
Shujaa Liyongo (2001), Mwepesi wa Kusahau (2005),
Masagisa na Zimwi Mbilikimo (2007) na Maadui wa
Maria (2007). Mwandishi ambaye amemaliza masomo
ya shahada ya M.A. kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, ni
mhariri na mfasiri wa habari katika Shirika la Habari la
Kenya, K.B.C.