Kichocheo Cha Fasihi
KSh550.00
Kichocheo cha Fasihi; Simulizi na Andishi ni kitabu kilichoandikwa kwa mtindo mwepesi na rahisi kusomeka. Kitabu hiki kinachunguza vipengele vya kimsingi vya fasihi simulizi na fasihi andishi kwa undani unaopatikana kwa nadra sana katika vitabu vilivyochapishwa.
100 in stock
Description

Kuna tofauti gani kati ya fasihi simulizi na andishi? Je, ni zipi tanzu kuu za fasihi simulizi? Je, ngomezi ni nini? Je, zipi tanzu kuu za fasihi andishi? Je, kuna tofauti gani kati ya fani na maudhui, dhamira na maudhui, ujumbe na falsafa?
Haya ni baadhi ya maswali yanayojibiwa kwa njia ya kuvutia na inayoeleweka vizuri sana. Mtindo wa Kichocheo cha Fasihi, pamoja na undani wake, unalifanya somo la fasihi kuwa na mvuto mkubwa na kuweza kueleweka vyema kuliko ilivyokuwa kabla. Ni kitabu cha lazima kwa wanafunzi na walimu katika shule za upili, vyuo vya ualimu na vyuo vikuu.
Dkt. K. W. Wamitila ni mhadhiri mkuu anayefundisha somo la Nadharia na Fasihi ya Kiswahili katika Chuo cha Elimu na Masomo ya Mbali (Kikuyu), Chuo Kikuu cha Nairobi. Baadhi ya vitabu vyake ni Uhakiki wa Fasihi; Misingi na Vipengele vyake, Bina-Adamul Zimwi la Leo (riwaya ya watoto) na English-Kiswahili AssortedDictionary{us Florence M. Kyallo). Vitabu vingine vitakavyochapishwa hivi karibuni ni; Kamusi ya Fasihi, Simba Mwamba na Safari ya Ajabu na Kovu la Jana.