Kurunzi ya Kiswahili: K.C.S.E Kitabu cha Marudio
KSh600.00
Sanja Leonard Leo, Mohammed Kusino
Kurunzi ya Kiswahili: K.C.S.E Kitabu cha Marudio kimeandikwa kwa madhumuni ya kuondolea mbali hali ya taharuki miongoni mwa wanafunzi na walimu kuhusu matarajio ya silabasi mpya. Yaliyopewa kipaumbele ni mahitaji ya mwanafunzi katika kuukabili mtihani wa sampuli yoyote ile.
100 in stock
Description
Waandishi wamepembua kwa mapana na marefu vipengele vyote vya silabasi mpya kwa njia sahili, fupi na rahisi kufuatia. Aidha, wametoa mifano ya karatasi za maswali zinazotoa taswira kamili ya mtihani wa K.C.S.E. Yote hayo yamefanywa kwa mtindo mufti ambao bila tashwishi utasadifu wanafunzi wa viwango vyote: wepesi darasani na wanaojifunza asteaste.
Baadhi ya vipengele muhimu vilivyoshughulikiwa kwa kina ni:
Uandishi wa insha
Ufahamu na ufupisho
Isimu-jamii
Matumizi ya lugha (sarufi)
Uchanganuzi wa sentensi
Fasihi simulizi na andishi
Uchambuzi wa vitabu teule (riwaya, tamthilia na hadithi fupi) pamoja na mashairi
Namna ya kujibu maswali ya sampuli zote.
Majaribio ya mitihani yenye sura tarajiwa ya K.C.S.E. silabasi mpya.
You must be logged in to post a review.
Reviews
There are no reviews yet.