Mayai waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine

KSh360.00

Mayai waziri wa Maradhi na Hadithi Nyingine ni diwani inayojumlisha hadithi fupi zinazoakisi
hall halisi katika jamii za Afrika Mashariki. Ni hadithi ambazo zinamfanya msomaji akereke na
kuungulika kwa kuiona dhiki, unafiki na uovu uliotamalaki katika matendo ya waja. Ni hadithi
zinazofichua uozo na uovu wa kisiasa, kiuchumi na kijamii; hadithi zinazokemea matendo
yasiyokuwa na uadilifu na zinazofichua uthori na ubaya ahasi ulioshamiri katika jamii zetu.

SKU: 9966-088-97-4 Category:

Description

Hadithi hizi ni kioo halisi cha kututazamisha jamii na kutufanya tutafakari kuihusu hatima
ya jamii yenyewe. Ni chocheo kubwa la fikira litakaloya- chokonoa mawazo ya wasomaji.
Diwani hit ni mchango aali kwenye utanzu huu muhimu. K.W. Wamitila, mhariri wa diwani hit, ni mwandishi maarufu aliyeandika vitabu vingi  vya fasihi na higha ya Kiswahili. Baadhi ya vitabu hivyo ni: Wingu la Kupita,  Pango (tamthilia), Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi, Kamusi ya Fasihi:Istilahi
na Nadharia na Kamusi ya Tashbihi, Vitendawili, Milio na Mishangao. Diwani ya mashairi
aliyoihariri, Tamthilia ya Maisha, itachapishwa hivi karibuni. Kwa sasa, Dkt. K.W. Wamitila
ni Mhadhiri Mkuu wa Somo la Fasihi na Nadharia katika Chuo cha Elimu na Masomo ya Mbali,
Chuo Kikuu cha Nairobi.