Mimba Ingali Mimba na Hadithi Nyingine

KSh340.00

Mimba Ingali Mimba na Hadithi Nyingine ni mkusanyo wa hadithi fupi uliofanywa kwa uangalifu mkubwa. Diwani hii imeleta pamoja hadithi fupi za aina tofauti kwa kuteua hadithi zenye mitindo na miundo mbalimbali. Ina maudhui yanayogusia matamanio, shida, fikra, falsafa kuhusu maisha, na vipengele vingi vya mazingira yanayoikumba jamii. Kupitia wahusika waliosawiriwa kwenye hadithi fupi zilizoko katika Mimba Ingali Mimba na Hadithi Nyingine, sherehe na milio ya waja inasimuliwa na waandishi stadi ambao wamenoa kalamu zao ili kuwasiliana na wasomaji kupitia nyanja hii ya fasihi.

SKU: 9966-01-059-9 Category: Tags: ,

Description

Owen MCOnyango ambaye ameuhariri mkusanyo huu ni mhadhiri katika Idara ya Isimu, Lugha na Fasihi katika Chuo Kikuu cha Maseno. Amefunza Kiswahili kwa miaka mingi katika Chuo hicho. Aidha, amefanya utafiti wa kina juu ya utanzu wa hadithi fupi na vilevile tanzu nyingine za fasihi ya Kiswahili. Mbali na kuandika makala ya kitaaluma MCOnyango hutunga pia mashairi.