Msimamo Kamili

KSh150.00

Msimamo Kamili
Mwandishi: Francis Taylor
Tafsiri: Angelina Mdari

SKU: ISBN 978 9966-882-57-X Category: Tags: ,

Description

Mtu yeyote anaweza kupatwa na UKIMWI. Wewe unaweza kupatwa na UKIMWI. Ili kuzuia ugonjwa wa UKIMWI usienee, ni lazima tuzungumze na tuzieleze habari za ugonjwa huu. Hii ndiyo sababu inayotufanya tuongee habari za UKIMWI sasa.
Pia, tunahitaji kuongea juu ya yale mambo yote mabaya ambayo watu wanayafanya. Mambo haya mabaya yanasambaza virusi vya HIV kwa watu wengi sana. Tutaweza kuzuia kuenea kwa UKIMWI kama tukiacha kuyafanya hayo mambo mabaya ambayo hueneza virusi. Vilevile tunahitaji kuongea juu ya njia zinazofaa za kuwatunza watu wetu wanaougua UKIMWI.
Watu wengine wamechanganyikiwa. Watu hao huongea mambo ya kijinga kuhusu kuonana kimwili kwa mume na mke. Usiwaruhusu watu hao wakubabaishe akili. Fanya ujasiri wa kuwaondokea. Waache. Visa na majadiliano yaliyomo ndani ya hiki kitabu yatakuongoza kujua jinsi ya kuwaepuka watu hao. Kwenye hadithi unazosimuliwa humu ndani, pengine unaweza kuona kisa kimojawapo ambacho kimekupata wewe mwenyewe au kimempata rafiki yako.