Mwavyaji wa Roho na Hadithi Nyingine

KSh360.00

Huu ni mkusanyiko unaoleta pamoja miwazo, hisia na fikira za waandishi mahiri kuhusu jamii. Ni juhudi za kuakisi ukweli wa hali halisi ilivyo na kuchorea msomaji taswira kamili kuhusu madhili ya uongozi, njaa, madawa ya kulevya na mahusiano ya kijamii kwa ujumla yaliyodorora. Wakati huo huo, wanamzidua juu ya mabadiliko; kuu likiwa kupatikana kwa katiba mpya.

SKU: 9966-01-157-9 Category: Tags: ,

Description

Huu ni mkusanyiko unaoleta pamoja miwazo, hisia na fikira za waandishi mahiri kuhusu jamii. Ni juhudi za kuakisi ukweli wa hali halisi ilivyo na kuchorea msomaji taswira kamili kuhusu madhili ya uongozi, njaa, madawa ya kulevya na mahusiano ya kijamii kwa ujumla yaliyodorora. Wakati huo huo, wanamzidua juu ya mabadiliko; kuu likiwa kupatikana kwa katiba mpya.

Waandishi basi hawakuzungumzia madhila tu ila wanapendekeza jinsi suluhu ya baadhi ya matatizo inavyoweza kupatikana. Tashtiti, maswali ya balagha na tashbibi zilizomshamiri katika nyingi za hadithi hizi zinadhihirisha uchungu, kero, dhiki na kiu ya waandishi; msumo wa kutaka kuhusika na kujihusisha na kupatikana kwa jamii bora. Waamini haya ndio matamanio ya wasomaji na jamii kwa jumla.