Mwendo

KSh190.00

Mwendo
Mwandishi: Elishi Lema

SKU: ISBN 978 9966-01-084-X Category: Tags: ,

Description

Kijijini Ruvula
Mtwara

Kwa Mpenzi Hamiata.

Je, hujambo? Mambo ya huku Mtwara ni mengi mno. Siwezi kukueleza yote kwenye barua hii. Halafu tena naiandika kwa haraka shangazi asije akanikamata. Karatasi yenyewe nimeichomoa kwenye daftari la watu.

Sasa sikiliza kwanza. Usiwe na wasiwasi. Yale madhara yalimtokea msichana wa Moshi vijijini hayatanitokea mimi, kwa hiyo tuliza roho yako mpenzi. Shangazi kaniambia kuwa kutahiri mtoto wa kike ni kama kuteka nyara haki yake ya kuwa mtu wa kike! Hamiata, sisi wasichana na wanawake wote kumbe tuna nguvu za uhai ndani mwetu! Sasa kutahiri mtoto wa kike ni kuvunja nguvu hizo na kuzinyima uhuru. Kwa hiyo shangazi kasema kwamba ni lazima sisi wasichana tukatae katu kufanyiwa hivyo. He! rafiki, nitakueleza mengi tutakapoonana…

Wako
Rafiki akupendaye sana
Felisia