Zinguo la Mzuka

KSh300.00

“Yote yalianza hapa kwenye madhabahu. Je, hatuwezi kuyajenga?”

Ujasiri, ari na azma inayozua michomo mikali ya kujipata upya pamoja na kurejesha urazini; inafanya watu waliozoea kukimya na kutazama madhabahu yao yakinajisiwa kufurukuta. Hii ni tamthilia inayoangazia maswala nyeti kama: ujenzi wa jamii mpya, uongozi, ukiritimba, ubinafsi na uozo mwingine wa kijamii. Isitoshe, inamulika uhusiano wa nchi huru za Kiafrika na nchi za Magharibi.

SKU: 9966-01-137-4 Category: Tags: ,

Description

“Yote yalianza hapa kwenye madhabahu. Je, hatuwezi kuyajenga?”

Ujasiri, ari na azma inayozua michomo mikali ya kujipata upya pamoja na kurejesha urazini; inafanya watu waliozoea kukimya na kutazama madhabahu yao yakinajisiwa kufurukuta. Hii ni tamthilia inayoangazia maswala nyeti kama: ujenzi wa jamii mpya, uongozi, ukiritimba, ubinafsi na uozo mwingine wa kijamii. Isitoshe, inamulika uhusiano wa nchi huru za Kiafrika na nchi za Magharibi.

Leo Sanja Leonard anatia guu tena katika uga wa fasihi na hii tamthilia inayozua hisia nzito. Mbali na kuwa mshairi, baadhi ya kazi zake ambazo zimechapishwa ni pamoja na; Mimba Ingali Mimba katika diwani ya Mimba Ingali Mimba na Hadithi Nyingine, Kasalia katika Shingo ya Mbunge na Hadithi Nyingine na Kurunzi ya Kiswahili.